Back to top

Rais Hassan Rouhani aionya Marekani.

23 July 2018
Share

Rais Hassan Rouhani wa Iran ameionya Marekani dhidi ya mgogoro wowote na Iran, akisema ni afadhali kwa Marekani kuepuka kuzusha vita vya kiuchumi na nchi yake.

Rais Rouhani amesema hayo katika mkutano na wajumbe wa wanadiplomasia wa Iran katika nchi za nje, na kuongeza kuwa Wamarekani wanapaswa kufahamu vizuri kuwa kupatana na Iran ni mwanzo wa amani yote, na kupambana na Iran ni mwanzo wa vita vyote.

Kufuatia uamuzi wa rais Donald Trump wa Marekani wa kujitoa kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya Iran tarehe 8, Mei, Marekani iliapa kurudisha tena vikwazo vilivyoondolewa kwa mujibu wa makubaliano hayo na kutoa adhabu kwa nchi zenye uhusiano wa kibiashara na Iran.

Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa itaufanya uuzaji wa mafuta ya Iran ushuke hadi "sifuri".