Back to top

Rais Magufuli aagiza wastaafu wa polisi walipwe ndani ya wiki moja.

26 February 2021
Share

Rais Dkt.John Magufuli ameiagiza Taasisi Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza shilingi bilioni 12 zilizokopwa na  Manispaa ya Temeke kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wake.

Ametoa agizo hilo alipokuwa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha ushonaji na uzinduzi wa majengo ya chuo hicho.

Amesema inashangaza kuona manispaa inakopa fedha katika benki za biashara na kufanya hivyo bila hata ya kuwa na kibali makhususi cha  serikali na huo ni utovu wa nidhamu.

Amesema kuna uwezekano kuwa fedha zimechukuliwa lakini kilichofanyika hakiendani na thamani halisi ya fedha, TAKUKURU ichunguze ili kufahamu undani wa matumizi yake.

Kabla ya Rais kutoa agizo hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Gerorge Simbachawene na Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro walimhakikishia Rais kuwa usalama unaendelea kuimarika hapa nchini.