Back to top

Rais Magufuli afanya mabadiliko ya uteuzi alioufanya

19 July 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Julai, amefanya mabadiliko ya uteuzi alioufanya tarehe 17 Julai 2020 ambapo amemteua Mhandisi Marwa Mwita Rubirya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Rubirya alikuwa meneja wa wakala wa barabara Tanzania(TANROADS) katika mkoa wa Mwanza.

Mhandisi Rubirya amemteuliwa badala ya Bw.Jumanne Fhika ambaye atabaki ofisi ya Rais kuendelea na majukumu yake.

Uteuzi wa Mhandisi Rubirya umeanza leo Tarehe 19 Julai 2020 na anatakiwa kuwepo Ikulu,Chamwino mkoani Dodoma kesho Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 saa 4:00 asubuhi.