Back to top

Rais Magufuli afungua kituo cha afya cha Madaba.

09 April 2019
Share

Rais Dkt. John  Magufuli amesema serikali itaendelea kujenga vituo vya afya na kwamba miradi mingi ya afya ilikua ikikwama kutokana na watu wachache kujinufaisha na fedha za miradi hiyo.

Rais Dkt. John  Magufuli ameyasema hayo wakati akifungua kituo cha afya cha Madaba kilichopo katika halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 665.