Back to top

Rais Magufuli akabidhiwa rasmi uenyekiti SADC

17 August 2019
Share

Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC unaendelea kufanyika hapa jijini Dar Es Salaam ambapo Rais Dkt.John Pombe Magufuli amekabidhiwa Uenyeketi wa Jumuiya hiyo kutoka Namibia.

Akifungua mkutano huo ambao umehudhuriwa na Marais 11 kutoka nchi mbalimbali wanachama wa SADC Rais Magufuli amesema ni fursa nzuri kwa watanzania kuendelea kulitangaza taifa kupitia mkutano huu wa kihistoria.

Akiongea kabla ya kukabidhi uenyekiti Rais wa Namibia Dkt.Hage Geingob amesema Tanzania ni nchi yenye amani na uchumi wake unaendelea kukua kwa kasi kubwa kutokana na utekelezaji wa miradi kubwa ya maendeleo ya kimkakati pamoja na uwekezaji katika viwanda kwa sasa ambao unachangia kupunguza tatizo la ajira hasa kwa vijana.

Dkt.Geingob amesema mafanikio ya maendeleo ya viwanda ni dira nzuri na mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama wa SADC hivyo ni fursa nyingine muhimu kwa nchi wanachama kujifunza kwa Tanzania na sasa wanaenda kuwa mwenyewkiti wa SADC kwa mwaka mmoja jambo ambalo ni historia nzuri.

Mwenyekiti huyo aliyemaliza muda wake pia ametangaza lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya nne inayotumika katika vikao mbalimbali vya jumuiya hiyo.

Mbali na Marais 11 kutoka nchi wanachama mkutano huo wa SADC wa leo na kesho unaendelea mpaka sasa umehudhuriwa na marais wote watatu wastaafu pamoja na Mawaziri wakuu wote wastaafu wa Tanzania na viongozi wengine waandamizi wa vyama mbalimmbali vya siasa.