Back to top

Rais Magufuli amemteua Mhe. Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mbeya

07 December 2018
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Taasisi za umma kama ifuatavyo.

1.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology – MUST).

2.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Zakia Hamdani Meghji kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST). 

3.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Esnati Osinde Chaggu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

4.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Samwel Gwamaka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

5.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Mej. Jen. Mstaafu Michael Isamuhyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

6.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Gaspar Stephen Mhinzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA).

Uteuzi wa viongozi hawa umeanza leo tarehe 06 Desemba, 2018.