Back to top

Rais Magufuli ameteua Mwenyekiti wa Tume ya utumishi wa umma.

04 December 2018
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji Mstaafu Steven Bwana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha miaka 3.

Pamoja na kumteua mwenyekiti wa tume, Mhe. Rais Magufuli amewateua
Makamishna 5 wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Walioteuliwa ni;
1. Bw. George D. Yambesi
2. Balozi Mstaafu John Michael Haule
3. Bi. Immaculate P. Ngwale
4. Bw. Yahaya F. Mbila
5. Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay.

Uteuzi huu wa Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa
Umma umeanza tarehe 22 Novemba, 2018.