Back to top

Rais Magufuli ampongeza Museveni kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru.

09 October 2018
Share

Rais wa Tanzania Mh. Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Rais Yoweri Museveni wa Uganda pamoja na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Taifa hilo.

Mh.Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter amemtumia salamu hizo za pongezi na kumuahidi Rais Museveni wa Uganda kwamba ataendelea kuukuza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Uganda. 

Katika ujumbe wa Rais Magufuli aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter amesisitiza kudumishwa kwa udugu, ujirani mwema na urafiki kwa manufaa ya Tanzania na Uganda.