Back to top

Rais Magufuli ampongeza Rais Mstaafu Mkapa kwa uongozi wake.

12 November 2018
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa uongozi. 

Mhe. Rais Magufuli ametoa pongezi hizo katika Misa Takatifu ya Shukrani ya uhai kwa Rais Mstaafu Mkapa ambaye leo tarehe 12 Novemba, 2018 ametimiza miaka 80 tangu kuzaliwa iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Upanga Jijini Dar es Salaam na kuongozwa Mwadhama Polycarp Kardinali.

Mhe. Rais Magufuli amesema wakati akiwa madarakani Rais Mstaafu Mkapa amefanya mambo mengi na muhimu kwa Taifa na amebainisha kuwa Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa kazi nzuri aliyoifanya.

Kwa upande wake Mhe. Rais Mstaafu Mkapa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumtakia heri, amewashukuru Maaskofu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mwandamizi Jude Thadaeus Ruwai’chi na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigirwa walioongoza Misa hiyo pamoja na viongozi wengine na waumini wenzake.