Back to top

Rais Magufuli amtumbua DED, DC kisha ateua.

19 October 2019
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Oktoba, 2019 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo.

1.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huo Bw. Kabunduguru alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu.

Bw. Kabunduguru anachukua nafasi ya Bw. Hussein Katanga ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

2.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Godfrey Gerald Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Elimu). Kabla ya uteuzi huo Bw. Mweli alikuwa Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Sheria na Katiba.

3.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Hashim Abdallah Komba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea. Kabla ya uteuzi huo Bw. Komba alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa.

Bw. Komba anachukua nafasi ya Bi. Rukia Muwango ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

4.    Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Hassan Abbas Rungwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.

Bw. Rungwa anachukua nafasi ya Bw. Bakari Mohammed Bakari ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.