Back to top

Rais Magufuli aongoza waombolezaji kuaga mwili wa Mercy Anna Mengi.

08 November 2018
Share

Rais John Magufuli na mkewe Janneth Magufuli wameungana na waombolezaji katika ibada ya kuuaga mwili wa mmoja wa waanzilishi wa Makampuni ya IPP, Mama Mercy Anna Mengi, katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ibada hiyo Rais Magufuli amewataka waombezaji kuiga mema ya Mama Mercy Anna Mengi.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt.Alex Malasusa ambaye pamoja na mambo mengine, amesema Mungu amewapa binadamu fumbo la kifo.

Akisoma wasifu wa Mama Mercy Anna Mengi, Bi.Heri Swai amesema alizaliwa tarehe 13.04.1948 katika K ijiji cha Wari Machame  Mkoani Kilimanjaro.

Pia katika ibada hiyo watu mbalimbali walipata fursa ya kutoa rambirambi zao kwa wafiwa na wengi walisema Mama Mercy Anna Mengi alikuwa ni mtu wa kujituma na mwenye kujishusha mbele ya watu.

Baada ya ibada ya kuuaga, mwili wa Mama Mercy Anna Mengi umepelekwa nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam ambako ibada zitaendelea na mwili wake utasafirishwa kesho kwenda Machame, Moshi kwa maziko.

Mama Mercy Anna Mengialifariki Oktoba 31, 2018 katika hospitali ya Medicinic Morningside, jijini Johannesburg, Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.

Maziko ya Mama Mercy Anna Mengi yatafanyika kesho kutwa, Machame Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe AMEN.