Back to top

Rais Magufuli ataka vituo vya kununulia dhahabu vianzishwe.

09 January 2019
Share

Rais  Dkt.John Pombe Magufuli ameitaka Wizara ya Madini na Tume ya Madini kuanzisha vituo vya kununulia dhahabu ili kubaini kiwango cha madini ya dhahabu kinachopatikana na kinachouzwa nje ya nchi.

Akizungumza katika halfa ya kuwaapisha Mawaziri, Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu wakuu wa wizara, Dkt.Magufuli amesema sekta ya madini bado inachangamoto kubwa kutokana na ripoti ya sasa kuonyesha Tanzania licha ya kuwa nchi yenye madini ya dhahabu mengi zaidi lakini haiongozi kuuza madini hayo nje ya nchi.

Aidha ameitaka wizara ya fedha, wizara ya madini kwa kushirikiana na Benki kuu waanze kununua dhahabu kwa mfumo wa kuwa na hifadhi ya dhahabu kama inavyofanyika katika dola ili kuwezesha watanzania kunufaika na rasimali zilizondani ya nchini yao.

Aidha Rais Dkt.Magufuli amesema katika Uongozi wake hatasitakufanya mabadiliko ya uongozi mara kwa mara iwapo ataona kuna mapungufu ya kiutendaji kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kuwaletea maendeleo watanzaia.

Awali akizungumza katika Hafla hiyo, Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema uteuzi wa viongozi hao utasaidia kuongeza nguvu ya kiutendaji ndani ya serikali ili kuhakikisha serikali inafikia malengo ya ilani ya CCM ya mwaka 2025.