Back to top

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti Bodi ya Mzinga na Mkuu wa Chuo cha NIT

07 November 2018
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Lut Jen. Mstaafu Samweli A. Ndomba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mzinga.

Lut Jen. Mstaafu Ndomba anachukua nafasi ya Bw. Andrew Severin Nyumayo ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Zacharia M.D. Mganilwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 05 Novemba, 2018.