Back to top

Rais Magufuli atumbua DC na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Malinyi

17 September 2019
Share

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro Bw. Majura Mateko Kasika na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bw. Mussa Elias Mnyeti.

Uteuzi wa viongozi hao umetenguliwa kuanzia leo tarehe 17 Septemba, 2019.

Uteuzi wa viongozi watakaojaza nafasi hizo utafanyika baadaye.