Back to top

Rais Magufuli awataka wananchi wa Katoro wakatae kubadilishwa mawazo.

15 July 2019
Share


Rais Dkt.John Pombe Magufuli amewataka wananchi wa mji mdogo wa Katoro na Buselele wilayani chato mkoani Geita kudumisha amani na kukataa kubadilishwa mawazo yao.

Akizungumza na wananchio hao,Dkt.Magufuli amesema amani ni kitu muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi na kuwataka kuchapa kazi ili kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano inayosisitiza watu kufanyakazi.

Kuhusu changamoto za miundombinu ya barabara, Rais Dkt.Magufuli amesema anatambua changamoto za barabara zinazoikabili eneo hilo na kusisitiza serikali inaanza ujenzi kwa awamu ikiwemo barabara kuu, barabara za mikoa na wilaya.

Amewataka kuchagua viongozi wasitoa rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi wa kumi mwaka huu ili waweze kusaidia kuleta maendeleo.

Aidha amewapongeza wananchi na idara ya misitu ya halmashauri ya wilaya ya chato kwa utunzaji wa misitu na kutaka kuendelea na utunzaji huo ili kuwezesha upatikanaji wa mvua.