Back to top

Rais Magufuli kuzindua nyumba za polisi Geita Julai 15.

13 July 2019
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaomba wananchi wa mkoa wa Geita pamoja na maeneo jirani na mkoa huo kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatatu kwenye tukio la uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari,uzinduzi utakaofanyika katika eneo la Magogo mkoani humo.

Aidha, IGP Sirro amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha askari wanaishi kwenye mazingira mazuri jambo ambalo litachangia weledi na uwajibikaji hususan kulinda maisha ya raia na mali zao.