Back to top

Rais Mstaafu wa Nigeria ampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri.

16 January 2019
Share

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Dkt. Olusegun Obasanjo  amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya katika uongozi wake ikiwemo kupambana na rushwa, kuimarisha utoaji wa elimu, kuimarisha miundombinu, kuongeza nishati ya umeme, kuboresha usafiri wa ardhini na angani na jinsi wadau mbalimbali wa ndani na nje wanavyopaswa kuelewa juhudi zinazofanyika.

Amezungumza hayo leo , baada ya kukutana na Rais Dkt.John Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Dkt.Obasanjo amesema Mhe. Rais Magufuli amedhihirisha kuwa kiongozi imara wa kusimamia mambo muhimu yenye maslahi kwa nchi yake na amebainisha kuwa licha ya kwamba maendeleo ya nchi hayapatikani mara moja lakini kwa muda mfupi Mhe. Rais Magufuli amefanya juhudi kubwa sana.