Back to top

Rais Mstaafu Mkapa asema lazima taifa lijitegemee

21 June 2018
Share

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa amesema ameanza kuwa na mashaka kwa namna ambavyo
Nchi imeanza kutegemea zaidi kupata misaada kutoka nje na kusema njia bora ni kuhakikisha nguvu
zinaongezwa katika watu kujiletea maendeleo kwa nguvu zao wenyewe.

Mh.Mkapa ameyasema hayo alipokuwa akizindua kitabu kinachoitwa Global Poverty kilichoandikwa na balozi
Mstaafu Matern Lumbanga jijini Dar es Salaam.

Naye mtunzi wa kitabu hicho mzee Lumbanga na amabye aliyiwahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi enzi za Rais
Mkapa amesema kitabu hicho kinaangazia zaidi hali umasini katika nchi moja na nyingine.

Walter Bgoya nimchapisaji wa kitabu hicho ambaye anasema kuna haja ya watu kubadilisha mtizamo
Kuhusu usomaji wa vitabu na badala yake wasome vitabu sana.