Back to top

Rais Samia awasili Zanzibar, kesho kuhudhuria maadhimisho ya Mashujaa.

06 April 2021
Share

Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amewasili Zanzibar akitokea Jijini Dar es Salaam ambapo hapo kesho atahudhuria maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) itakayofanyika katika Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Mhe. Rais Samia amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na baadaye amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi.