Back to top

Rais Samia azungumza kwa njia ya simu na Rais wa Benki ya AFDB.

11 June 2021
Share

#PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya simu masuala mbalimbali ya kimaendeleo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dkt. Adesina Akinwumi ambaye alikuwa akizungumza kutokea Makao Makuu ya Benki hiyo Abidjan nchi Ivory Coast.

Kupitia mazungumzo hayo Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AFDB Dkt. Adesina Akinumwi amemhakikishia Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kuwa benki hiyo itaendelea kufadhili miradi ya maendeleo hapa nchini na ipo tayari kufadhili miradi mipya kwa kuwa Tanzania ina sifa za kuendelea kupata ufadhili.