Back to top

Rais Uhuru Kenyatta atangaza UKAME kuwa janga la taifa Kenya.

10 September 2021
Share

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameutangaza ukame ambao umeathiri baadhi ya sehemu za nchi hiyo kuwa janga la taifa, ukame huo umeathiri watu milioni mbili wa kaunti kumi kati ya 47 za nchi hiyo.
.
Rais Kenyatta amezungumza kauli hiyo baada ya mkutano na viongozi wa eneo lililoathirika Kaskazini mwa nchi hiyo, ambako hawajapata mvua kwa muda mrefu.
.
Ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani iwasaidie waathiriwa wa janga hilo ambao ni wafugaji wanaokabiliwa na njaa na wanyama wao wanakufa, serikali imesema itachukua hatua madhubuti kukabiliana na ukame huo.