Back to top

Rais Uhuru Kenyatta azindua sarafu mpya jijini Nairobi.

11 December 2018
Share

Sarafu mpya zisizokuwa na picha za rais yeyote zimeanza kusambazwa kwa matumizi nchini Kenya hii leo.
 
Ni baada ya benki kuu kuchapisha sarafu hizo zilizowekwa picha za wanyamapori na nembo zingine za kitaifa kama ilivyoratibiwa kwenye katiba. 

Akizungumza baada ya uzinduzi wa sarafu hizo Rais Uhuru Kenyatta katika benki kuu ya Kenya jijini Nairobi anasema uwepo wa sarafu hizo mpya kutawawezesha wakenya wote kuhisi uzalendo wao.