Back to top

Rais wa Somalia asaini Sheria ya kumfanya aendelee kusalia madarakani.

15 April 2021
Share

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmaajo ametia saini sheria ya kuongeza muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili.

Hatua hiyo inafuatia bunge kuidhinisha hoja ya kuongeza muda hali iliyoibua mzozo uliosababisha kuchelewa kufanyika kwa uchaguzi.

"Rais Mohamed Abdullahi Farmajo amesaini rasmi sheria ya maalumu ya uchaguzi Jumanne jioni. Bunge lilipitisha kwa kura nyingi muswada huo siku ya Jumatatu"-Waziri wa Habari Osmani Dubbe ameeleza.

Muda wa kukaa madarakani kwa Farmajo ulikwisha tarehe 8 mwezi Februari huku bunge likiwa limemaliza muda wake tangu mwezi Disemba- uchaguzi wa wabunge na rais uliokuwa ukipaswa kufuata ulikumbwa na mizozo ya kisiasa.

Viongozi wa upinzani wa Somalia na wa majimbo ya Jubbaland na Puntlandpia baraza la seneti , walikataa uamuzi wa bunge.

Wafadhili wa Somalia, zikiwemo Marekani na Umoja wa Ulaya wamepinga uamuzi huo.