Back to top

Rais wa Zamani wa Algeria Abdelaziz Bouteflika afariki.

18 September 2021
Share

Rais wa zamani Algeria Abdelaziz Bouteflika afariki dunia, televisheni ya taifa hilo imesema Abdelaziz aliyeiongoza Algeria kwa miongo miwili kabla ya kujiuzulu 2019 kufuatia maandamano makubwa ya kupinga muhula wa tano, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka themanini na minne.
.
Bwana Bouteflika aliondoka madarakani Aprili 2019 chini ya shinikizo kutoka jeshini, kufuatia majuma  kadhaa ya maandamano ya kupinga azma yake ya kuwania muhula wa tano madarakani.
.
Baada ya kujiuzulu, hakuonekana tena hadharani na kusalia kwenye makazi yake Mashariki mwa mji mkuu wa Algiers.
.
Bouteflika alichaguliwa rais wa Algeria mwaka 1999 wakati koloni hilo la zamani la Ufaransa likitoka kwenye vita vya muongo mmoja vilivyosababisha vifo vya watu karibu laki mbili.