Back to top

Rais wa zamani wa Chile ateuliwa kuwa Kamishna mkuu haki za binadamu.

09 August 2018
Share

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amemteua Rais wa zamani wa Chile Bi. Michelle Bachelet kuwa Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja huo akichukua nafasi ya Bw. Zeid Ra'ad Zeid Al-Hussein atakayemaliza muda wake mwishoni mwa mwezi huu.

Bibi Bachelet aliwahi kuwa Rais wa Chile kwa mihula miwili, na ni rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Chile. Pia alikuwa mkurugenzi mtendaji wa kwanza wa Shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2013.