Back to top

RC Katavi aiagiza TAKUKURU kumkamata afisa ushirika.

14 June 2019
Share

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bwana.Juma Homera ametoa agizo la kukamatwa kwa afisa ushirika wa wilaya ya Mlele Bwana.Joseph Malima na kuchunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatia taarifa za afisa huyo kuhusika kushinikiza Jeshi la Polisi kuwaachia wafanyabiashara waliokuwa wamekamatwa kwa kununua Tumbaku ya daraja la kwanza zaidi ya kilo 20,000 kwa njia za magendo yenye thamani ya shilingi milioni 120 sanjari na kutoa saa 48 kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kufanya msako wa kukamata walanguzi wa Tumbaku.
  
Ametoa agizo hilo kufuatia taarifa ya chama cha msingi cha wakulima wa Tumbaku Ukonongo alipokutana na wakulima hao na kukagua ghala la kuhifadhia Tumbaku, ambapo pia alilazimika kuendesha zoezi la kupiga kura za siri kutambua majina ya walanguzi wa Tumbaku.
  
Awali wakitoa taarifa viongozi wa chama cha msingi Ukonongo wamesema pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo ni uuzaji wa Tumbaku kwa njia za magendo unaofanywa na wakulima wasio waaminifu.
 
Naye mrajis wa vyama vya ushirika mkoa wa katavi amesema kitendo cha kuuza Tumbaku kinyume na utaratibu wa stakabadhi ghalani kunadhoofisha mapato ya mkoa husika.