Back to top

RC Rombo awaonya vijana wanaokunywa pombe kupindukia.

04 August 2020
Share

Mkuu wa Wilaya ya Rombo Dkt.Athuman Kihamia amewaonya vijana wa wilaya hiyo waache kunywa pombe kupindukia na kutumia dawa za kulevya vitendo ambayo vinaathiri afya zao na nguvu kazi ya taifa katika uzalishaji.

Dkt.Kihamia ametoa onyo hilo wakati anakabidhi pikipiki kwa kikundi cha vijana waendesha bodaboda cha Huruma cha wilaya hiyo iliyotolewa na ofisi yake na kueleza kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiidhalilisha wilaya ya Rombo.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rombo Bw.Godwin Chacha amesema halmashauri hiyo itaendelea kuvikopesha vikundi ambavyo vinafanya vizuri ktk urejeshaji na kuvionya vinavyosuasua.

Ofisa Maendeleo ya Vijana wa wilaya hiyo Edwin Wilson amesema asilimia themanini na tano ya shilingi milioni mia moja tisini na sita nukta tano ya mikopo iliyotolewa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu wa wilaya ya Rombo tangu 2017 hadi mwaka huu, imerejeshwa.