Back to top

'Royal Tour' Wawekezaji waanza kumiminika Tanzania.

22 September 2021
Share

Makala ya kutangaza vivutio vya utalii, biashara na uwekezaji iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo itaoneshwa kwenye kipindi maarufu cha Royal Tour, imeanza kuzaa matunda baada ya wawekezaji kujitokeza kwa ajili ya uwekezaji wa hoteli za kisasa ndani ya Hifadhi za Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Damas Ndumbaro ametoa kauli hiyo mara baada ya mkutano wake maalum na Wawekezaji uliofanyika Dar es Salaam, ambapo amekutana na wawekezaji hao kutoka Bara la Ulaya katika nchi ya Bulgaria watakaojenga hotel zenye hadhi ya Nyota tano 'Brand' za Kempinski kwenye hifadhi Nne za Taifa nchini.

Dk.Damas Ndumbaro amesema mpango mkakati wa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kuandaa kipindi cha Royal Tour umeweza kuzaa matunda hayo na wao kwa Wizara wameupokea kwa kwa sasa ni utekelezaji.

"Juhudi kubwa za kimkakati za Royal Tour zilizoendeshwa na Rais wetu zimeweza kuzaa matunda ambapo leo tumepokea wawekezaji mahiri kutoka Bara la Ulaya ambao watawekeza kwenye hoteli kwa kujenga hoteli tatu za nyota tano za 'Brand' ya Kempinski kwa uwekezaji wa Dola za Kimarekani Milioni 72. [USD 72 Milioni].

"Mkutano wetu huu hii leo umekwenda vizuri sana na Wawekezaji hawa  kwa hiyo unaweza kuipata hoteli ya Kempinski baada ya ujenzi huo kukamilika. .. Kempinski Serengeti,  Kempinski Manyara, Kempinski Tarangile na Kempinski Ngorongoro." Dk.Ndumbaro.