Back to top

Rugemalira, Seth na Mwakandege wakwama kumaliza kesi yao kupitia DPP.

06 May 2021
Share

Aliyekuwa Mwanasheria wa kampuni ya  kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Mwakandege, ameondoa rasmi maombi yake ya kufanya majadiliano ya kuimaliza kesi.
.
Mwanasheria huyo amefikia hatua hiyo baada ya siku 45 zilizotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya mshtakiwa huyo kuisha bila yeye kuonana wala kufanya majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania(DPP).
.
Mwakandege kupitia wakili wake, Alex Balomi ameieleza Mahakama hiyo Mei 6, 2021, wakati kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili yeye na wenzake wawili ambao ni Harbinder Seth na James Rugemalira, ililipoitwa kwa ajili ya kutajwa.
.
Mwakandege na Seth waliandika barua za kukiri mashtaka yao na kuomba kupunguziwa adhabu ili waimalize kesi yao.