Back to top

Ruzuku sio kigezo cha chama cha siasa kuwa na nguvu ya kushika dola.

01 July 2020
Share


Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Bwana Mohamed Ahmed amesema ruzuku sio kigezo cha chama cha siasa kuwa na nguvu ya kushika dola, badala yake amevitaka vyama hivyo vijenge hoja na ushawishi kwa wananchi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba mwaka huu.

Ahmed amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu vyama vya Siasa nchini havina budi vijitazame na kujikosoa kwa hoja zilizo imara zenye uwezo wa kuwashawishi wanachama wake katika msingi wa kushika dola, baada ya kutazama ruzuku, kwani wakati wa kuanzisha mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992, vyama hivyo havikuwa na uwezo wa kifedha.

Aliongeza vyama voyte vyenye usajili wa kudumu vina haki sawa kwa mujibu wa sheria na kuwa hata vyama vyenye uwezo wa ruzuku  vimejikuta vikiingia katika migogoro ya mara kwa mara na kuathiri dhana ya msingi mkuu wa vyama vya siasa, ambayo  ni kushika hatamu ya uongozi na kuongoza dola.