Back to top

Sakata la kuapishwa wabunge 19 viti maalum CHADEMA lapamba moto.

26 November 2020
Share

Baraza la Vijana la CHADEMA (Bavicha) limeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoa maelezo ya orodha ya makada wake 19 walioapishwa hivi karibuni bungeni kuwa wabunge wa viti maalum kwamba imetoka wapi.

Mwenyekiti wa BAVICHA John Pambula amesema baraza hilo linaunga mkono msimamo wa CHADEMA juu ya mwanachama wa chama hicho kwenda kinyume na mwongozo wa chama.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti huyo amesema kutokana na chama hicho hakikupitisha majina ya wabunge hao wa viti maalum na wala Katibu wa hakuwahi kusaini kuonyesha chama hicho kimeteua hivyo ni vema NEC ijitokeze hadharani na iseme majina waliyoyapitisha walipewa na nani.