Back to top

Sanamu ya mwanajeshi aliyeshika bunduki kivutio cha utalii Ruvuma.

14 February 2019
Share

Sanamu kubwa ya  mwanajeshi aliyeshika bunduki  katika makumbusho ya mashujaa wa vita vya majimaji iliyojengwa kwa ajili ya kuwaenzi wanajeshi waliopigana vita vya  Kagera  imekuwa kivutio  kikubwa cha utalii mkoani Ruvuma.

Akizungumza na ITV Muhifadhi kiongozi wa makubusho ya vita vya maji maji Bw. Baltazari Nyamusya amesema sanamu hiyo ina mafundisho makubwa  chini yake ikiwa na maandishi yanayosomeka sisi mababu zenu mashujaa wa  majimaji tumetoa maisha yetu kutetea taifa letu,tumetimiza wajibu wetu  uliobaki ni wenu.