Back to top

Serengeti Boys yaiadhibu Morocco bao moja kwa nunge.

14 November 2020
Share


Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys iliyopo nchini Morocco kwa ajili ya kujiwinda na michezo ya kuwania kifuzu michuano ya AFCON leo imeshinda mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Morocco kwa bao 1-0.

Katika mchezo wa leo mchezaji Ladaki Juma aliyekuwa katika Serengeti Boys iliyopita ambaye kwasasa ni nahodha wa Serengeti Boys ya sasa ameibuka mchezaji Bora wa mechi.

Timu hizi za Vijana kati ya Wenyeji Morocco na Serengeti Boys zitarudiana tena tarehe 17 mwezi huu kabla ya Serengeti Boys kurejea nyumbani Tanzania.

Akizungumza na ITV kocha wa timu hiyo Maalim Salehe amesema kuwa atahitaji michezo ya kirafiki tena nyumbani Tanzania kabla ya kwenda Rwanda kwa ajili mechi za kufuzu AFCON kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17.