Back to top

Serikali imesema imepiga hatua kubwa katika sekta ya afya nchini.

13 November 2018
Share

Serikali imesema imepiga hatua kubwa katika sekta ya afya ambapo sasa upasuaji mkubwa ambao ulikuwa ukifanyika nje ya nchi unafanyika hapa hapa nchini na kuliokolea taifa fedha.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema hayo Bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu hoja zilizoelekezwa kwa wizara hiyo katika muongozo wa mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Amesema upasuaji huo ni ule wa upandikizaji wa figo ambapo ilikuwa ikigharimu shilingi milioni mia moja na ulikuwa ukifanyika nchini India lakini sasa unafanyika kwa shilingi milioni thelathini hapahapa nchini.

Bunge limepitisha muongozo wa mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20.