Back to top

Serikali imetenga hekari 217000 kwa ajili ya kuwawezesha vijana.

09 August 2018
Share

Serikali imetenga hekari 217000 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kushiriki shughuli za kilimo huku halmashauri zikiagizwa kuandaa program maalum za kilimo biashara katika maeneo yao ili kuhamasisha kundi hilo ambalo ni zaidi ya asilimia 60 ya watanzania kushiriki kufanikisha mpango wa taifa wa uchumi wa kati wa kilimo na viwanda.

Hekari hizo limetengwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira na vijana Anthony Mavunde anasema serikali pia imeandaa mikakati ya kubadilisha mtazamo wa vijana juu ya kilimo kuwa hakina tija na kuendelea kutenga maeneo maalum ya kilimo na kuwawezesha vijana kupata mitaji na fursa.

Wakati serikali ikiweka mikakati hiyo kwa maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla ITV inazungumza na vijana wa jiji la Dodoma kama wanazitambua fursa hizo na wameomba kuwepo na uwazi katika utekelezaji wake pamoja na viongozi waliopewa dhamana kuisimamia kuwajibika.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mavunde amekabidhi pikipiki ya magurudumu matatu kwa kijana mlemavu Dominic Lembele mwanafunzi uhandisi wa computer Chuo Kikuu cha Dodoma ambaye anawataka vijana wenye changamoto kama yake kutokata tamaa ya maisha bali wajitokeze ili waweze kutambuliwa na kusaidiwa.