Back to top

Serikali inapata Bilioni 80 kwa mwezi tozo za miamala, mitandaoni.

23 January 2021
Share

Serikali imesema shilingi Trilioni kumi nanane zinapita kwenye mitandao kwa mwezi.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.Faustine Ndugulile amesema hayo jijini Dodoma katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kilichohudhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo na wakuu wa taasisi zake.

Dkt.Ndugulile amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa miamala milioni mia tatu inafanyika kwa mwezi mtandaoni na serikali inapata shilingi bilioni themanini kwa mwezi za tozo kutokana na fedha zinazopita mtandaoni na mzunguko huo wa fedha mtandaoni kwa mwezi.

Amesema Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ni njia kuu ya uchumi na inawezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano yenye kasi, kufanikisha utendaji kazi wa mifumo ya TEHAMA na huduma za fedha mtandaoni.