Back to top

Serikali kuendelea kudhibiti mimba kwa wanafunzi.

09 April 2019
Share

Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania limeambiwa kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti mimba kwa wanafunzi ili kuhakisha kuwa wanafunzi wote wanakamilisha elimu yao bila kikwazo chochote.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Tekinlojia  Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu swali la Mhe.Asha abdulaha Juma Mbunge wa Viti Maalum CCM aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kuhakisha inakabiliana na ongezeko la wasichana kupata mimba na kukatisha masomo.

Mhe.Olenasha amesema katika kukabilina na ongezeko la wasichana wanaokatisha shule kwa sababu za mimba serikali ilifanya marekebisho   ya sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978.

Akaongeza kuwa marekebisho hayo ya mwaka 2016 mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari atahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

Naibu Waziri huyo akasema kuwa huduma za ushauri na unasihi hutolewa kwa wanafunzi ambapo mwongozo wa ushauri na unasihi umeandaliwa vilevile mafunzo mbalimbali juu  ya stadi za maisha elimu ya afya na uzazi hutolewa kwa wanafunzi.