Back to top

Serikali kufanya tathimini ya wagonjwa wa Fistula nchini.

23 May 2018
Share

Serikali kupitia wizara ya afya  imeweka wazi mpango wake wa kufanya tathimini nchini nzima ili kujua idadi kamili ya wanawake wanaokabiliwa na wagonjwa wa fistula ili kuweza kurahisisha uratibu wa matibabu ya upasuaji kwa wagonjwa hao ambao wengi wao wako pembezoni mwa nchi.

Watalaam wa afya wanasema moja ya visababishi vya ugonjwa wa fistula ni uzazi pingamizi, na mimba za utotoni ambapo kwa mwaka 2016 pekee zaidi wanawake wenye fistula 1000 walipatiwa matibabu na kwa mujibu wa UNFPA wanasema matukio ya fistula 1200 hadi 3000 yamekuwa yakiripotiwa hapa nchini huku wadau wa afya wakisema ni muhimu huduma za afya ya mama na mtoto zikazidi kuimarishwa hasa maeneo ya pembezoni mwa nchi.

Serikali inasema ni muhimu kwa wanawake wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya ikiwa ni pamoja na kuhudhulia cliniki kwa wakati ambapo sasa tayari vituo vya afya 200 zimeanza kufanyiwa ukarabati ili kutoa huduma za mama na mtoto kote nchini.

Kila ifikapo May 23 kila mwaka Tanzania huungana na nchi zote ulimwenguni kuadhimisha siku ya fistula lengo ikiwa ni kuhakikisha jamii inaondoka na dhana ya unaynyapaa kwa wagonjwa wa fistula ambayo sasa inatibika pasi na gharama yoyote.