Back to top

Serikali kuhakikisha wahitimu wa vyuo wanapata ajira.

23 May 2018
Share

Serikali inamikakati ya kuhakisha wahitimu wa vyuo wanapata ajira za kuajiriwa na kujiajiri ambapo moja ya mikakati hiyo ni kusimamia utekelezaji wa sera ya uchumi wa viwanda.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Ajira,Kazi na Vijana Anthony Mavunde wakati akijibu swali la Mhe.David Silinde Mbunge wa Momba aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kuongeza ajira.

Mh Mavunde akasema kuwa serikali inatekeleza miradi mikubwa nchini ikiwemo mradi wa bomba la mafuta,ujenzi wa reli ya kisasa  na ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa nishati kupitia miradi mbalimbali ambayo  yote kwa ujumla itasaidia kupanua wigo wa nafasi za ajira.

Aidha akaongeza mkakati mwingine ni  kuendeleda kuwezesha vijana kujiajiri kwa kuwapatia mikopo yenye msharti  nafuu kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana.

Mh Mavunde akasema kuwa serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa program ya taifa ya kukuza ujuzi ambayo  itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha vijana kuajirika na kupunguza tofauti ya ujuzi iliyopo kati ya nguvu kazi  na mahitaji ya soko la ajira.