Serikali imesema kuwa imeamua kuifanya shule ya msingi ya Mwisenge iliyopo Musoma mkoani Mara aliyosoma Baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa shule ya kihistoria ikiwa ni sehemu moja wapo ya kumuenzi baba wa taifa huku ikitoa zaidi ya milioni 780 kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo.
Hayo yameelezwa na Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Musona na kutembelea shule hiyo inayoendelea kukarabatiwa.
Waziri mkuu amesema kuwa shule hiyo ya Mwisenge itaubeba mkoa wa Mara kwa kuwa na historia ya vongozi wakubwa kupitia shuleni hapo.