Back to top

Serikali kujenga jengo la utengamano na mazoezi tiba kwa watoto.

15 February 2019
Share

Serikali imeahidi kujenga jengo la utengamao na mazoezi - tiba kwa watoto wenye ulemavu katika vituo vya afya 510 vinavyomilikiwa na serikali ili kuimarisha huduma za matibabu na kuwafikia watoto hao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Mhe.Ummy Mwalimu, katika ufunguzi wa kituo kipya cha utengamao na mazoezi-tiba kwa watoto wenye ulemavu cha kila siku, Based Rehabilitation Jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu amekiri kuguswa na mchango wa kina mama wenye watoto wenye ulemavu na kuwataka kutumia mfuko wa watu wenye ulemavu kuomba mikopo isiyokuwa na riba ili kuwezesha familia zao na kujikimu katika maisha.

Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini, Mhe.Roberto Mengoni na Mkuu wa Shirika la Comsol, Bwana Michelangelo Chiurchiu wamesema kukamilika kwa mradi huo ni ndoto iliyotimia kutokana na kiu kubwa ya kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu nchini.