Back to top

Serikali kujenga viwanda vya Dawa nchini

21 August 2018
Share

Serikali chini ya mpango wa sekta ya umma na binafsi ipo katika mchakato wa ujenzi wa viwanda vikubwa vya dawa katika mikoa ya Mbeya,Mwanza na Dar es Salaam  ili kupunguza gharama na hasara ya kuagiza bidhaa hiyo kutoka nchi mbali mbali ikiwemo  India kwa lengo la kuongeza kasi ya upatikanaji wake.

Akizungumza na ITV jijini Tanga huku wizara ya fedha na mipango kwa kushirikiana na benki ya dunia wakianza mchakato wa kushirikisha sekta ya umma na binafisi katika zoezi la kuimarisha uchumi,afisa afisa uhakiki ubora bohari kuu ya dawa nchini Twahiri Magori amesema hivi sasa wapo katika hatua ya upembuzi yakinifu kisha baadae watatangaza tenda kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Awali naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango Suzan Mkapa pamoja na mkufunzi wa mpango wa (PPP) kutoka benki ya dunia Ned White wamesema mchakato wa zoezi la (PPP) limesaidia katika miradi mingine ya kitaifa na kimataifa hivyo ni vyema wadau wakatilia mkazo ili mipango ya serikali iweze kufikiwa.