Back to top

Serikali kumuenzi Nyerere kupambana na umaskini, maradhi na ujinga.

09 October 2019
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kapteni Mstaafu  George Mkuchika amesema serikali itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kupambana na vita alivyovianzisha dhidi ya umaskini, maradhi na ujinga.

Mhe.Mkuchika amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wakiwemo walionufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF na kwamba Tanzania inapokumbuka miaka ishirini ya kifo cha baba wa taifa Marehemu Mwalimu Nyerere vita dhidi ya maradhi,umaskini na ujinga vinaendelea kupiganwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kapteni Mstaafu  George Mkuchika.

Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo Bwana.Aden Nchimbi amesema mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF umesaidia kupunguza umaskini katika wilaya ya namtumbo na kuongeza hasama ya wananchi kufanya kazi za kujipatia kipato.

Baadhi ya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini wamesema kwa kiasi kikubwa mpango huo umewasaidia kuondokana na umaskini ambapo wameweza kufungua biashara za kujitegemea ikiwemo genge migahawa na kujenga nyumba za bati.