Back to top

Serikali ya China imeridhia kufadhili ujenzi wa Chuo cha anga.

25 March 2019
Share

PICHA NA MAKTABA.

 

Serikali ya China imeridhia kufadhili  ujenzi wa Chuo cha kwanza  cha anga hapa nchini  kitakachotoa mafunzo ya urubani kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro hatua  inayotajwa kuimalisha ufanisi wa shirika la ndege Tanzania ATCL kwa kupata marubani wazalendo wataozalishwa hapa nchini.
 
Mkuu wa Chuo cha  taifa  cha usafirishaji kilichopewa jukumu la kusimamia chuo hicho  cha urubani Prof. Zacharia Mganilwa anasema chuo hicho cha kwanza tangu Tanzania ipate uhuru kimepangwa kujengwa kwenye eneo la uwanja wa KIA kwakuwa upo karibu na viwanja  vya Moshi,Tanga na Arusha ambako wanafunzi itakuwa rahisi kufanya mazoezi ya vitendo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro Mhandisi Christopher Mkoma anasema tayari wawakilishi kutoka nchini China wameshafika na  wamerizika na mazingira ya eneo hilo.