Back to top

Serikali ya India yaweka utaratibu ya Visa zilizo Isha muda wake.

29 March 2020
Share

Balozi wa Tanzania nchini India Mhe.Baraka Luvanda amesema Watanzania wote wanaoishi India wakiwemo wanafunzi na wagonjwa waliokwenda kwenye matibabu hawajapata maambukizi ya Covid 19 na usalama wao ni wa hali ya juu.

Kwa mujibu wa mtandao wa worldometers unaofuatilia matukio yanayotokea duniani kwa kila sekunde Mpaka kufikia leo Machi 29, 2020 India imepata maambukizi ya wagonjwa wa virusi vya Corona 987 huku idadi ya vifo ikifikia watu 25.

Balozi Luvanda ameeleza kuwa India pekee ni nchi ambayo ni kubwa na inaidadi kubwa ya watu wanaofikia bilioni 1.3 hivyo nchi hiyo imejipanga vyakutosha kuthibiti ugonjwa wa COVID19 nchini humo.  

Mwanahabari wetu Agnes Almasy amezungumza kwa njia ya video na Balozi Luvanda kuhusu usalama wa wanafunzi Watanzania waliopo nchini humo katika vyuo mbalimbali amesema wapo salama na hawajapata maambukizi ya COVID19 na kuhusu Visa za wanafunzi ambazo zimekwisha amesema serikali ya nchi hiyo imeweka utaratibu mzuri ndani ya kipindi hiki cha katazo cha siku 21 watu wataongezewa muda wa Visa bila malipo.
 
Kuhusu kusambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha askari wa Kihindi wakiwachapa bakora raia wa nchi hiyo ambao wamekaidi agizo la serikali yao kukaa ndani kipindi hiki cha Corona Balozi Luvanda amesema waliokuwa wakitandikwa bakora walikaidi agizo la serikali ya nchi hiyo la kuwataka wananchi nchini humo kukaa ndani katika kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID19.  

Balozi luvanda ambaye pia anahudumu nchi za Singapore, Nepal, Bangladesh na Syrilanka amesema jitahada mbalimbali wameendelea kuzifanya huku akitoa ushauri kwa watanzania wote waishio India.