Back to top

Serikali ya Zanzibar kuongeza bajeti ya Elimu.

27 September 2020
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein amesema serikali itaendelea kuongeza bajeti ya elimu kwa vile inaridhika na matumizi ya fedha hizo ambazo zimekuwa zikililetea faida ya kuinua kiwango cha elimu Zanzibar.

Dkt.Shein ametoa kauli hiyo Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na wanafunzi wa kidato cha nne na sita waliofanya vizuri mitihani ya kitaifa nchini ambapo amemsmea kiwango cha ufaulu kimeongezeka na bajeti itaendelea kuongezwa.

Amesema anamaliza mudawake wa uongozi mwezi ujao na kuwatoa hofu wazazi na wananchi kuwa serikali itafuata misingi hiyo hiyo huku waziri wa elimu Mhe.Riziki Pembe Juma akisema Dkt.Shein atakumbukwa kwa vile amechangia sana elimu hasa kukubali kuwalipia wanafunzi  masomo ya nje.

katika hafla hiyo Dkt.Shein aliwatunuku zawadi mbali mbali wanafunzi waliofanya vizuri.