Back to top

Serikali yaandaa mpango wakukabiliana na watu wanaowasumbua wakulima

02 July 2020
Share

Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe amesema Serikali imeandaa mpango wa kuondoa madalali waliojikita katika sekta ya Kilimo ambao wanatumia sekta hiyo kwa malengo yao mengine yakiwemo ya kupata mikopo na kuwaacha wakulima wakiendelea kuteseka.


Naibu waziri Bashe amesema hayo Mkoani Arusha katika ziara yake ya kutembelea wakulima na wadau wa kilimo,huku akiwataka watendaji wa ngazi zote kuwasaidia wakulima hasa wadogo kuondokana na uonevu wanaofanyiwa.