Back to top

Serikali yadhibiti uhalifu na utekaji magari Kigoma

16 June 2018
Share

Uongozi wa mkoa wa Kigoma kupitia mkuu wake wa mkoa Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga umeseMa serikali imedhibiti uhalifu na utekaji magari katika barabara kuu zinazotoka nje ya mkoa wa huo kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa wananchi hali inayosababisha wananchi kusafiri kwa usalama.

Brigedia Jeneral Maganga ameyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga katika baraza la Eid Ujiji Mjini Kigoma, ambapo amesema serikali itaendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu.

Akaongeza kuwa ili kuhakikisha Kigoma na nchi inakuwa salama lazima kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao bila ya hofu wala mashaka.

Kwa upande wake Shekh wa mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika zoezi linaloendelea la uandikishaji vitambulisho vya taifa huku akiitaka serikali kuwadhibiti baadhi ya watu wanaopotosha juu ya zoezi hilo na kusababisha watu kutojitokeza