Back to top

Serikali yafafanua kuhusu kusitishwa matangazo ya uzazi wa mpango.

20 September 2018
Share

Serikali imesema haijasitisha huduma wala elimu ya uzazi wa mpango bali kwa sasa wamesitisha matangazo ya uzazi wa mpango kwa muda kwenye vyombo vya habari  ili kuyapitia upya  na kuhakikisha maudhui yanayoifikia jamii yanakuwa na muonekano ambao serikali imekusudia.

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndungulile katika mahojiano maalum na ITV.