Back to top

Serikali yafunga migodi yote iliyofukia wachimbaji Mkoani Geita.

10 May 2020
Share

Siku moja baada ya wachimbaji watano wa dhahabu kufukiwa na mgodi huku mmoja kufariki dunia na watatu wakinusurika kifo wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji dhahabu katika migodi ya Magema Mkoani Geita serikali imefunga migodi yote katika eneo hilo.

Serikali pia imewataka wachimbaji  zaidi ya elfu moja waliokuwa wakichimba kinyemela kuondoka katika eneo hilo.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo Mkaguzi wa Migodi na Baruti kutoka Ofisi ya Madini Mkoa wa Geita, Mhandisi Martini Shija amesema wamelazimika kuwaondoa wachimbaji wote na kuifunga migodi yote kutokana na wachimbaji hao kuvamia eneo la mwekezaji kinyemela na kusababisha maafa.

Wakizungumzia hatua iliyochukuliwa na serikali kuwaondoa katika eneo hilo wachimbaji hao wameiomba serikali kuwapa muda kutokana na uwekezaji waliowekeza na pia kuwatafutia maeneo salama ya uchimbaji ili waendelee kujikimu na umasikini.